Loading...

WANAFUNZI ZAIDI YA 22 WAPOTEZA MAISHA SUDAN

Loading...
Wanafunzi 22 wamekufa maji baada ya boti lao kuzama Jumatao wiki hii kwenye mto Nile, katika mkoa ulio kwenye umbali wa karibu kilomita 750 kaskazini mwa mji wa Khartoum, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Zaidi ya watoto 40 kwa jumla walikuwa wakisafiri na boti hilo.

Wanafunzi hao walikuwa wakienda shuleni wakati wa tukio hilo, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna, ambalo pia limeripoti kifo cha mwanamke mmoja, na watu 23 waliojeruhiwa katika tukio hilo.

Ajali kama hizi zimekua zikitokea kwenye mto Nile nchini Sudan na kusababisha raia kuwa na wasiwasi wa kusafiri kupitia mto huo.
Na Haika Gabriel.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WANAFUNZI ZAIDI YA 22 WAPOTEZA MAISHA SUDAN WANAFUNZI ZAIDI YA 22 WAPOTEZA MAISHA SUDAN Reviewed by By News Reporter on 8/16/2018 08:06:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.