Loading...

MANENO NA LUGHA UNAYOTUMIA KILA SIKU YANA NGUVU KUBWA KATIKA MATOKEO YA MAISHA YAKO

Loading...
Kuna siri kubwa imejificha katika nguvu ya MANENO na LUGHA tunazotumia katika maisha yetu. Maneno unayotumia kila siku  yana nguvu ya kutengeneza uhalisia ambao unaweza kuwa una faida au hasara katika maisha yako inategemea na neno lenyewe.

Toka unaamka asubuhi hadi jioni unatumia maneno gani kuelezea maisha yako na ya wengine? Je ni maneno yenye kukutia nguvu na hamasa ya mafanikio au ni maneno yenye kukukatisha tamaa na kukuondolea matumaini ya mafanikio ndani yako?. 

Ni vyema kutathmini kila neno kabla ya kutamka, mara nyingi tumeumba aina ya maisha tunayoishi leo kutokana na maneno yetu. 

LUGHA unayotumia kuelezea maisha yako ina athari katika mafanikio yako. Jifunze kutumia maneno CHANYA yatakayokuongezea ujasiri, nguvu, hamasa, motisha na matumaini ya kufanikiwa. 

You Deserve The Best!
Vicent Stephen
MANENO NA LUGHA UNAYOTUMIA KILA SIKU YANA NGUVU KUBWA KATIKA MATOKEO YA MAISHA YAKO MANENO NA LUGHA UNAYOTUMIA KILA SIKU YANA NGUVU KUBWA KATIKA MATOKEO YA MAISHA YAKO Reviewed by By News Reporter on 8/16/2018 07:51:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.