Hivi karibuni kijana mmoja wa Indonesia aliokolewa baharini baada ya kupotea huko kwa muda wa siku 49 akiwa katika mtumbwi wake wa kuvulia samaki.
Lakini cha kustaajabisha Aldi Novel Adilang alitaarifu kuwa hiyo haikuwa mara yake ya kwanza kuokolewa baharini.
Adilang, 18, amewahi kuokolewa kwa namna ya kushangaza si kwa mara moja pekee bali mara tatu.
Ingawa wakati huu habari ya kupotea kwake imeweza kufahamika zaidi duniani kwa sababu alikuwa katika eneo la mbali.
Kijana huyo aliyekuwa anafanya kazi ya kuvua katika mtumbwi wake ambao kina muonekano wa kibanda, kilikuwa kinaonekana kikielea katikati ya bahari huku kikiwa kimefungwa Kamba.
Tarehe 14 Julai, Adilang alikuwa amefunga kamba kilomita 125 pembezoni mwa fukwe ya bahari ili kuweza kuvuta kiota chake wakati wa kuvua samaki.
Adilang anasema kiota chake kiliharibika baada ya rafiki yake kukisafisha.
Anasema hakufahamu wakati ambao alipoteza uelekeo,
"Nilikuwa nimelala hivyo sikujua kama nilikuwa napoteza uelekeo,siku chache za mwanzo , chakula nilichokuwa nimebeba kwnye chombo changu kilinisaidia lakini kiliisha ndani ya wiki moja tu.
Hivyo mchele,maji safi,viungo na vitu vingine viliisha .
Ili niweze kuendelea kuishi ilinibidi niwe navua samaki na kuchoma sehemu ya kiota changu ili kuweza kuwasha moto wa kupikia na niliwahi kula hata samaki bila kumpika".
Changamoto nyingine ambayo alikutana nayo ilikuwa ni kupata maji safi.
Hivyo katika kutafutia suluhisho la jambo hilo alizilowesha nguo zake na kunywa maji ya baharini kwa kutumia nguo kwa madai kuwa nguo yake ilikuwa inachuja maji kuwa safi na kupunguza ladha ya chumvi ya maji ya bahari.
Katika siku 49 akiwa anaelea katika maji, zaidi ya meli 10 zilipita katika eneo alilokuepo na hakuna iliyemuona.
Loading...
1mf _1mj" data-offset-key="esbfa-0-0" style="direction: ltr; position: relative;">
"Nikiwa peke yangu katikati ya bahari nikiimba nyimbo za dini na kusoma biblia ambayo nilikuwa nimeibeba huku nikiendelea kusali sana, nikiwa na matumaini ya kuwaona wazazi wangu tena".
Aidha kijana huyo alikiri kuwa kuna wakati alipatwa na msongo wa mawazo na alitamani kujizamisha mwenyewe baharini lakini maombi aliyokuwa anayafanya yalimpa nguvu ya kuwa na matumaini ya kuokolewa.
"Tarehe 31 Agosti ,niliiona meli iliyokuwa imebeba nishati za kupikia.
Wakati huo nilikuwa nnalia na kusema nisaidie nisaidie,yani hicho ndio kitu pekee nilikuwa nakifahamu kwa wakati huo na kwa bahati nzuri wafanyakazi wa meli hiyo waliniona na kuniokoa.
Kitu cha kwanza walifanya baada ya kuniokoa walinipa maji na kunibadilisha nguo"
Adilang anasema alikaa kwenye meli hiyo kwa muda wa wiki moja mpaka ilipofika mwisho wa safari nchini Japan.
Alipowasili Japan tarehe 6 september alirudi kwao Indonesia baada ya siku mbili na kujumuika na familia yake
Adilang anasema mara mbili alizokwama baharini zilichukua muda mfupi zaidi.
Mara ya kwanza ilichukua wiki moja na kusaidia na mmiliki wa boti na mara ya pili ilikuwa siku mbili na vilevile alipata msaada kutoka kwa mmiliki wa boti.
Akiwa katika chombo chake cha kuvulia hakua na vitendea kazi vyovyote vya kuonyesha ishara ya anakoelekea zaidi ya tochi ambayo ilikuwa imebuniwa kuwavutia samaki.
Kila wiki kijana huyu alikuwa anavua samaki ambazo zilichukuliwa na kampuni aliyokuwa anafanyia kazi .
Adilang alikuwa katika mkataba wa mwaka mmoja ambapo alikuwa analipwa dola 134 kila mwezi .
Lakini baada ya tukio hili , Adilang amehaidi kuwa hataenda tena kuvua.
Na Hussein Juma.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
APOTEA BAHARINI KWA MWEZI NA NUSU KABLA HAJAOKOLEWA
Reviewed by By News Reporter
on
9/29/2018 07:11:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: