Loading...

BOBI WINE AISHUTUMU SERIKALI YA MUSEVEN KWA MAUAJI YA AFISA WA POLISI

Loading...
Siku kadhaa baada ya afisa wa polisi wa ngazi ya juu Muhammed Kirumira kuuawa, Bobi Wine, ambaye jina lake kamili Robert Kyangulanyi alishutumu serikali kwa mauaji ya afisa huyo.

Katika ujumbe alioandika Facebook, Bobi Wine aliomboleza kifo cha afisa huyo aliyekuwa na miaka 35 pekee wakati wa mauaji yake.

"Ndugu yangu Afande Kirumira, leo unazikwa ukiwa na miaka 35 pekee. Mpaka sasa sijaamini kuwa uliuawa ukiwa hauna uwezo wa kujitetea. Makosa yako yalikuwa kusema ukweli na kupigania haki pamoja na kupenda taifa lako. Hawakuwa na huruma," alisema katika ujumbe huo.

Afisa huyo alikuwa anapendwa sana nchini Uganda hasa kwa kupigania haki za wanahabari, ambao mara kwa mara walikuwa wakinnyanyaswa na maafisa wa polisi wakiwa katika kazi zao.

Marehemu aliuawa pamoja na mkewe aliyekuwa ameafuatana naye ndani ya gari lake Jumamosi karibu na nyumbani kwake, Bulenga, Wilaya ya Wakiso.

Wauaji wake walisemekana kuendesha pikipiki wakati wa kisa hicho. Kabla ya mauaji yake, na alikuwa ametangaza kupokea vitisho.

Afisa huyo alisimamishwa kazi Januari kama kamanda wa polisi wilayani kwa kushutumu wenzake kuhusiana na kuhusika katika ufisadi na kushirikiana na makundi ya kihalifu. 

Bado Bobi Wine anazidi kutibiwa Marekani baada ya kudhulumiwa na kuumizwa na maafisa wa polisi karibu mwezi mmoja uliopita.
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BOBI WINE AISHUTUMU SERIKALI YA MUSEVEN KWA MAUAJI YA AFISA WA POLISI BOBI WINE AISHUTUMU SERIKALI YA MUSEVEN KWA MAUAJI YA AFISA WA POLISI Reviewed by By News Reporter on 9/11/2018 10:00:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.