Loading...
Mwanzilishi na kiongozi wa kanisa la Ghana's International God’s Way Church pasta Daniel Obinim aliibua hisia baada ya video yake kusambaa mitandaoni.
Kwenye video hiyo, inadaiwa kuwa pasta huyo alitaka kupaa hadi mbinguni akiwa katika tawi mojawapo la makanisa yake.
" Nahisi kupaa sasa….nahisi kupaa," alisikika akisema.
" Mnitazame, niko karibu kutoweka," aliongezea.
Obinim aliwaagiza waumini wanase video huku akijitayarisha kupaa kuelekea mbinguni.
Baadhi ya mapasta wake pamoja na waumini walimzunguka upesi na kumsihi asipae na kuwaacha duniani.
Licha ya pasta huyo kuwaahidi kuwa angerudi baadaye kutoka mbinguni, waumini hao walimsihi wakisema kuwa wakati haukuwa umefika wa yeye kuwaacha.
Hii si mara ya kwanza ambapo pasta huyo anaripotiwa kujaribu kupaa, katika kisa kingine cha awali, pasta huyo aliyekuwa amevalia suti alionekana akiyafungua mikono yake sawa na ndege tayari kupaa.
Nabii huyo ambaye anapingwa vikali na baadhi ya watu wasiomuamini kwa miujiza yake ni kati ya mapasta matajiri zaidi nchini Ghana. Tazama video hiyo hapa: https://youtu.be/fvDNLhrYKHM
Na Andrew Daniel.Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HIVI NDIVYO PASTA OBINIM WA GHANA ALIVYOJARIBU KUPAA MBINGUNI
Reviewed by By News Reporter
on
9/12/2018 01:52:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: