Loading...

INDONESIA YAKUMBWA TENA NA TSUNAMI

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi lililoandamana na tsunami imefikia 832 nchini Indonesia.

Janga hilo lililotokea katika kisiwa cha Sulawesi limesababisha kupotea kwa watu wengine 29.

Watu takriban elfu kumi na saba wamehamishwa makazi yao.

Kumekuwa na uhaba wa chakula,maji na huduma mbovu ya umeme kutokana na tetemeko hilo.

Rais Joko Widod
Loading...
ameamuru vikosi vya jeshi vitumwe katika maeneo yaliyoathirika ili kusaidia katika shughuli za uokoaji.

Mamlaka ya hali ya hewa ya Indonesia inalaumiwa kwa kuchelewa kutoa angalizo kwa sababu onyo juu ya tsunami lilitolewa ndani ya saa moja kabla ya tsunami kupiga.

Inakumbukwa kuwa mwaka 2004 tsunami ilisababisha tetemeko la ardhi nchini Indonesia na watu zaidi ya laki mbili walifariki.

Mwaka 2010 pia zaidi ya watu 282 waliuawa na tsunami iliyosababishwa na tetemeko la ardhi katika pwani ya Sumatra nchini Indonesia.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
INDONESIA YAKUMBWA TENA NA TSUNAMI INDONESIA YAKUMBWA TENA NA TSUNAMI Reviewed by By News Reporter on 9/30/2018 11:11:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.