Loading...
Mgahawa mmoja wa Maine maarufu kwa kutengeneza chakula kinachotokana na Lobster wamebuni mbinu ya kuwavutisha bangi viumbe kabla ya kuwapika au kuwaua, wakiamini ni kitendo cha kibinadamu zaidi, kwa maana wanawapunguzia maumivu.
Katika jaribio, Charlotte Gill mmiliki wa mgahawa wa Charlotte Legendary Lobster, aliwaweka lobster kadhaa katika sanduku na maji machache na kisha moshi wa bangi ulipulizwa ndani ya sanduku hilo, mtandao wa WMTW iliripoti.
Gill, ambaye ni mtoa huduma wa bangi mwenye leseni katika jimbo la Maine, alidai kuwa lobster walikuwa watulivu kwa kipindi cha wiki tatu zilizofuata na hata kuamua kuwaruhusu tena baharini.
"Nahisi vibaya kwamba wakati lobster wakifikishwa hapa hawana namna yoyote ya kuondoka," Gill alimwambia Mount Desert Islander.
Gill alisema ni vigumu kwa binadamu kulewa kutokana na bangi aliyopuliziwa lobster wakati wa kumpunguzia maumivu kabla ya kuuliwa na kupikwa.
Mgahawa huu umekuwa wa kwanza kuja na mbinu ya kibunifu, ambapo unafaa kuwa mfano wa kuigwa hata kwa wanyama wengine kama ng'ombe, mbuzi na kuku wakati wa kuchinjwa.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

LOBSTER KUVUTISHWA BANGI KABLA YA KUPIKWA
Reviewed by By News Reporter
on
9/22/2018 09:36:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: