Loading...

MAMIA WALAZWA HUKU 27 WAFARIKI KWA POMBE ILIYOHARIBIKA

Loading...
Watu 27 wafariki na wengine 302 walazwa hospitali kwa kunywa pombe iliokwishaharibika  nchini Iran.

Pombe hiyo ilikuwa imekwishaharibi kwa kuwa muda wake wa kutumiwa kama kinywaji ulikuwa umekwishapita.

Unywaji wa pombe  nchini Iran umepigwa marufuku tangu mageuzi ya kiislamu nchini humo mwaka 1979.

Pombe huuzwa kimagendo nchini humo na mara nyingine hutengenezwa majumbani na katika warsha.

Kulingana na sheria nchini humo,muuzaji na mnunuaji wa pombe hupewa adhabu ya kifungo na kupigwa fimbo.

Jeshi la Polisi limefahamisha kuwakamata watu wawili wanaoshukiwa kuuza pombe hiyo ilioharibika.

Adhabu kali hutolewa  dhidi ya watu wanaokamatwa  kwa makosa ya kunywa pombe.
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAMIA WALAZWA HUKU 27 WAFARIKI KWA POMBE ILIYOHARIBIKA MAMIA WALAZWA HUKU 27 WAFARIKI KWA POMBE ILIYOHARIBIKA Reviewed by By News Reporter on 9/30/2018 11:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.