Loading...
Mapato ya sekta ya utalii yameongezeka kwa asilimia 13.6 katika mwaka wa serikali ulioishia Juni 2018, uliosababishwa ongezeko kubwa la wimbi la watalii, kutokana na mipango ya pamoja ya masoko iliyotekelezwa na sekta za umma na binafsi.
Serikali ilikusanya jumla ya Dola $2,403.2 milioni (Sh5.44 trilioni) mwaka ulioishia mwezi Juni 2018, kutoka dola 2,115.6 iliyokusanya mwaka jana wakati kama huo huo, takwimu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonyesha.
"Hii ilikuwa ni kutokana na kuongezeka kwa wasafiri wa utalii baada ya juhudi za makusudi za kutangaza vivutio vyetu vya utalii kufanywa na sekta binafsi na umma," BoT ilisema katika mapitio ya kiuchumi ya mwezi Julai 2018.
Takwimu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii zinaonyesha kwamba Tanzania ilivuta wageni karibu milioni 1.3 mwaka 2017, kutoka milioni 1.3 mwaka 2016.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii wa Tanzania (TTB), Devota Mdachi aliiambia gazeti la The Citizen jana kuwa idadi ya shughuli za utangazaji zimeongezeka kwa asilimia 60 mwaka ulioisha Juni 2018 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, anaishukuru serikali kuongeza bajeti ya TTB.
"Tumefanya shughuli nyingi za utangazaji. Tuliwaalika waandishi wa habari kutoka China, Japan na Uturuki ambao walitembelea nchini na kuandika habari kuhusu nchi yetu ambayo tunaamini ilisaidia kuvuta wageni zaidi," alisema.
Kulingana na maelezo yake, mwaka 2017/18 bodi hiyo ilihudhuria maonyesho 14 ya kimataifa ambapo ilitumia fursa ya kukuza vivutio vya utalii na kukutana na mawakala wa utalii duniani.
Lengo la mwaka huu, alisema, ni kuhudhuria maonyesho 22 ya kimataifa pamoja na matukio yaliyoandaliwa ikiwa na pamoja 4th Swahili International Tourism Expos kati ya mengine.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KWA 13.6%, BoT INAONYESHA
Reviewed by By News Reporter
on
9/07/2018 09:20:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: