Rais John Magufuli leo Septemba 5, amekutana na Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania Mzee Pius Msekwa na mkewe Mama Anna Abdallah katika Ikulu Ndogo ya Nansio Ukerewe mkoani Mwanza.
Akizungumza wakati wa watatu hao walipokutana, Msekwa alimpongeza Rais Magufuli na kusema amefanya mageuzi makubwa yanayoandika historia kama alivyofanya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
“Kwa Nyerere tulisema kama si juhudi zako Nyerere, maendeleo tungepata wapi, na huyu Rais Magufuli naye tutasema kama sio juhudi zako meli, Dreamliner, reli na mengine mengi tungepata wapi?” amesema Msekwa.
Ameipongeza Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kisiwani humo ikiwamo maji, ujenzi wa barabara na ununuzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria.

Loading...
tyle="font-family: "verdana" , sans-serif;">
Baada ya mazungumzo yao Mzee Msekwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kufanya ziara yake ya kwanza katika kisiwa cha Ukerewe tangu achaguliwe kuwa Rais.
Kwa upande wake Mama Anna Abdallah amemshukuru Rais Magufuli kwa kazi kubwa ya kujenga uchumi na kuwapa nafasi za uongozi wanawake wengi.
Pia Mama Anna Abdallah ametoa wito kwa wanawake wote waliopata nafasi za uongozi kuonyesha mfano mzuri kwa kuchapa kazi kwa juhudi, uadilifu mkubwa na kujiamini ili wengine wengi zaidi waendelee kupata nafasi.
“Nafurahishwa sana na kazi zinazofanywa na Rais Magufuli, kwa hakika anatutendea mazuri mengi sana sisi Watanzania na sisi wanawake” amesema.
Na Haika Gabriel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

SPIKA MSEKWA AMFANANISHA MAGUFULI NA JK NYERERE
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
9/05/2018 12:29:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: