Staa wa muziki wa Hip Hop Bongo Joh Makini maarufu kama Mwamba wa Kaskazini kutokea kundi la Weusi amefunguka na kutaja sababu zilizomsukuma kutoa wimbo wa Injili.
Joh Makini amesema sababu kubwa iliyomfanya mpaka kuimba wimbo wa gospel ni kuonyesha ni Kwa jinsi gani Mungu ana maana kubwa maishani mwake.
Kwenye mahojiano na gazeti la Risasi Vibes, Joh Makini alisema kwamba wimbo huo kwake ni ‘Hip Hop Gospo’ wenye ujumbe ‘strong’ na si mwisho wa kuimba nyimbo za namna hiyo, ataend
Loading...
lea kila anapopata idea kwa sababu Mungu ni kila kitu kwake.
"Hakuna ambaye hafahamu kwamba Mungu ni kila kitu kwenye maisha ya binadamu, nimeimba wimbo huu ili kufikisha ujumbe kwa mashabiki zangu kufahamu kwamba suala la Mungu kutufanikisha kwenye maisha yetu si la kumwachia yeye tu.
"Sisi pia tunatakiwa kupambana kwa namna zetu na yeye anabariki nia zetu na kufanya tupate kila tunachotamani".
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JOH MAKINI AFUNGUKA SABABU ZA KUTOA WIMBO WA INJILI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
9/05/2018 12:04:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: