Loading...

BASATA WATANGAZA ZAHAMA KWA MREMBO SANCHOKA

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limetoa tamko kuwa litamshughulikia mwanamitindo ambaye ni gumzo mtandaoni kwa kuposti picha za nusu utupu, Jane Rimoy ‘Sanchi’ baada ya malalamiko ya watu wengi ya kwa nini baraza hilo halimchukulii hatua kama ambavyo hufanya kwa wengine.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Afisa Habari wa Basata, Agnes Kimwande alisema kwanza hawamtambui Sanchi kama mwanamitindo na hawajui ni kazi gani maalum ambayo anaifanya ndiyo maana walisita k
Loading...
mchukulia hatua ila watafuatilia kama ni kweli anajihusisha na kazi za sanaa ili wamchukulie hatua mara moja na sio kwamba wanamuogopa.

“Watu wengi wanatumia kivuli cha sanaa kufanya mambo ambayo kimsingi sio mazuri sio kwamba tunamuogopa kumchukulia hatua, hapana ila sisi hatumtambui huyo Sanchi kama ‘Model’, kwa sababu sisi tunamchukulia hatua mtu ambaye anafanya makosa kwenye kazi ya sanaa mfano Diamond akivua nguo akiwa anafanya shoo tutamshughulikia kwa sababu inatuhusu sisi moja kwa moja ila naahidi tutamfuatilia kama kweli anafanya sanaa ili tujiridhishe kama anatuhusu basi tutamshughulikia,” alisema Agnes.
Na Julian Zomba.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BASATA WATANGAZA ZAHAMA KWA MREMBO SANCHOKA BASATA WATANGAZA ZAHAMA KWA MREMBO SANCHOKA Reviewed by By News Reporter on 10/26/2018 07:51:00 AM Rating: 5

Maoni 1 :

Inaendeshwa na Blogger.