Loading...

TUZO MBADALA YA NOBEL YANYAKULIWA NA WASAUDI ARABIA

Loading...
Wanaharakati watatu wa haki za binadamu kutoka Saudia walioko jela watunukiwa tuzo mbadala ya Nobel na taasisi ya Nobel mjini Stockholm. Pia wapinga rushwa kutoka Guatemala watunukiwa tuzo ya heshima.

Washindi wa tuzo maalum ya haki za binadamu au tuzo mbadala ya Nobel wametangazwa leo hii mjini Stockholm Sweden. Tuzo hiyo imetunukiwa watetezi watatu wa haki za binadamu wakisaudi waliofungwa jela pamoja na wanaharakati wa kupinga rushwa kutoka Amerika Kusini.

Taasisi ya tuzo hiyo mjini Stolkholm imesema dolla 113,400 zinazoambatana na tuzo hiyo mbadala ya Nobel zitagawanywa kwa washindi Abdullah al Hamid,Mohammad al-Qahtani na Waleed Abu al Khair wote wa Saudi Arabia kutokana na juhudi zao za kijasiri zinazosimamia misingi ya haki za binadamu ya kimataifa,ili kuleta mageuzi katika mfumo wa kidhalimu wa kisiasa nchini Saudi Arabia.

Tuzo  ya heshima ya mwaka huu imetunukiwa Thelma Aldana wa Guatemala na mkolombia Ivan Velasquez kutokana na mchango wao mkubwa katika kuyafichua matumizi mabaya ya mamlaka pamoja na uozo wa rushwa.

Tuzo ya Right Livelihood ambayo pia inajulikana kama tuzo mbadala ya Nobel ni tuzo inayotolewa kila mwaka  tangu ilipoanzishwa mwaka 1980 na mwanahisani Jakob von Uexkull raia wa Sweden mwenye asili ya Kijerumani kwa lengo la kuwatunuku watu wanaoendesha juhudi ya kupigania haki za binadamu duniani wanaohisiwa kupuuzwa au kutopewa nafasi katika tuzo za Nobel.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
TUZO MBADALA YA NOBEL YANYAKULIWA NA WASAUDI ARABIA TUZO MBADALA YA NOBEL YANYAKULIWA NA WASAUDI ARABIA Reviewed by By News Reporter on 9/25/2018 08:40:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.