Loading...

USWISS YATUPILIA MBALI MAOMBI YA BILIONEA ABRAMOVICH

Loading...
Mamlaka nchini Switzerland imetupilia mbali maombi ya kuishi nchini humo kutoka kwa bilionea wa Kirusi Roman Abramovich.

Bilionea huyo ni mmiliki wa klabu ya mpira ya Chelsea ambaye alituma maombi yake ya kutaka kuishi maeneo ya mapumziko ya Alpes ya Verbier, ambapo awali alikubaliwa , lakini polisi wa shirikisho la Uswisi walitoa sababu ya kukataa ombi hilo kuwa wanahisi Abramovich anaweza kuhatarisha usalama na hivyo basi ombi lake likatupiliwa mbali.

Mpaka sasa hakuna ushahidi wowote wa kihalifu alioutenda, na mwanasheria wa Abramovich amesema kwamba madai hayo wanayomshukia yote ni ya uongo.

Abramovich anatuhumiwa kwa uhalifu wa kutakatisha fedha na makosa mengine ya jinai yote hayo bado hayajathibitishwa, lakini mamlaka nchini Uswis imetamka bayana kuwa hazihitaji ithibati; hisia kidogo tu juu yake zinatosha kuwa sababu ya kusitisha maombi yake ya ukaazi.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
USWISS YATUPILIA MBALI MAOMBI YA BILIONEA ABRAMOVICH USWISS YATUPILIA MBALI MAOMBI YA BILIONEA ABRAMOVICH Reviewed by By News Reporter on 9/26/2018 10:39:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.