Loading...
Ziwa Ngosi linalopatikana Mbeya, mojawapo ya maajabu yake ni ukilitazama kwa juu lina muonekano halisi kama ramani ya Afrika, na visiwa vya Pembana Unguja vinaonekana pia.
Katika Ziwa Ngosi kwa juu maji yake ni baridi, lakini ukizama chini maji ni moto.
Licha ya kukariwa kuwa na kina cha mita 74 kwenda chini, unaambiwa kuwa kina hicho hubadilika mara kwa mara, hivyo akili yako wewe fanya kama unahisi kina ni mita 74 lakini usijaribu kukipima kina hicho.
Hakuna kabisa samaki katika Ziwa Ngosi, kwa sababu ni yamechanyika na kusababisha hewa ya oksijeni isipatikane kabisa. Ukitaka kuogelea uwe na moyo wa chuma maana ni kama unataka kuogelea katika maziwa freshi.
Wakazi wa maeneo ya karibu na Ziwa Ngosi, hutumia maji yake kama dawa ya ngozi na pia wanaamini maji hayo huondoa mikosi ambapo imani hizo zilikuwepo tangu muda na zipo, kabla hujapanda utakuta baadhi ya watu wakiuza maji ya ziwa hilo.
Hakuna mto unaoingia au kutoa maji katika Ziwa Ngosi, maji yametulia tu mfano kama maji yapo kwenye bakuli. Hayapungui wala kuongezeka.
Maji ya Ziwa Ngosi hubadilika rangi kila mara, unaweza leo ukakuta ya Bluu, kesho Meusi n.k. Kwa sababu ni kutokana na msitu na pia upande wa jua na mawingu yatakavyokaa kwa siku hiyo.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

FAHAMU MAAJABU YA ZIWA NGOSI
Reviewed by By News Reporter
on
10/07/2018 03:01:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: