Loading...

KOMANDO ROBOW AZUILIWA KUWANIA UONGOZI SOMALIA

Loading...
Komando wa zamani na mwanzilishi wa kundi la wanamgambo wa kiislamu nchini Somalia ,Mukhtar Robow, amezuiliwa kuwania uongozi serikalini.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, wizara ya usalama imesema kuwa bwana Robow hawezi kuwania wadhifa wowote serikalini kwasababu bado anakabiliwa na vikwazo vya kisheria.

Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya Robow kutangaza kuwa atawania uraisi wa jimbo la kusini magharibi katika ichaguzi ujao wa kimaeneo.

Mukhtaar Robow amesema uamuzi wake wa kuingia katika siasa unafuatia wito wa wananchi, wafuasi wake katika jimbo hilo la kusini magharibi.

Amedhihirisha kwamba yupo tayari iwapo atashinda, kuidhinisha uhusiano thabiti na serikali ya shirikisho katika mji mkuu Mogadishu, ambayo imekuwa katika mzozo na tawala za baadhi ya majimbo.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KOMANDO ROBOW AZUILIWA KUWANIA UONGOZI SOMALIA KOMANDO ROBOW AZUILIWA KUWANIA UONGOZI SOMALIA Reviewed by By News Reporter on 10/06/2018 07:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.