Loading...

WATANZANIA WATANO WADAAKWA KENYA WAKIPELEKWA ARABUNI

Wasichana watano wa Kitanzania wamekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) mjini Nairobi wakiwa katika harakati za kusafirishwa kwenda Oman na raia wa Kenya aliyefahamika kwa jina la Geoffrey Manzi.

Walionaswa walikuwa miongoni mwa wasichana saba waliokuwa wakisafirishwa na Manzi, huku wengine wawili wakiwa raia wa Uganda. Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi imethibitisha kukamatwa kwa Manzi akiwa JKIA akijiandaa kuwasafirisha wasichana hao isivyo halali.

Taarifa ya DCI kwa vyombo vya habari ilisema Jumanne iliyopita, makachero walimvamia mtu huyo anayedaiwa kufanya biashara ya kusafirisha binadamu akiwa katika mchakato wa kuondoka na wasichana saba wakiwamo Watanzania watano na Waganda wawili. "Wasichana hao waliokolewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta wakijiandaa kuondoka nchini (Kenya) kwenda Oman," alisema DCI.
Loading...
font-family: Verdana, sans-serif;">
Tukio hilo limetokea wakati Idara ya Uhamiaji nchini ikiwa imesitisha utoaji wa vibali vya kazi vya kazi kwa Watanzania wanaokwenda kufanya kazi zisizo rasmi nje ya nchi. Uhamiaji ilifafanua kwamba lengo la utaratibu huo ni kuwakinga Watanzania wanaokwenda kufanya kazi hizo dhidi ya vitendo vya kikatili wawapo ughaibuni.

Akizungumzia tukio hilo, Msemaji wa Uhamiaji nchini, Ally Mtanda alisema zuio hilo bado linaendelea, lakini hakuwa na taarifa za Watanzania hao kukamatwa na mamlaka za Kenya.

"Sina taarifa hizo, tunatarajia kupokea taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, tuliweka zuio kwa wanaokwenda kufanya kazi zisizo rasmi, bado linaendelea," alisema.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WATANZANIA WATANO WADAAKWA KENYA WAKIPELEKWA ARABUNI WATANZANIA WATANO WADAAKWA KENYA WAKIPELEKWA ARABUNI Reviewed by By News Reporter on 10/03/2018 06:42:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.