Loading...
WATU wanaokadiriwa kuwa idadi 3,000 ndani ya vijiji 11 vinavyozunguka mgodi wa kuchimba madini ya dhahabu ACACIA ulipo Nyamongo wilayaniu Tarime mkoani Mara wanatarajiwa kunufaika na upimaji wa macho bure.
Kaimu meneja wa mgodi wa ACACIA,Festo Shayo alisema juzi katika uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa macho bure ilioandaliwa na mgodi huo kuwa wanatarajia kupima watu 3000 katika kampeni hiyo.
“Tunaamini kwamba Afya ni nguzo mhimu katika maendeleo kwa kila jamii kwa hali hiyo tunataka ifike mahala kila moja atambue wajibu wake wa kiafya kwa kupima ili ukae ukijua Afya yako”alisema Shayo.
Kama mdau wa maendeleo nchini Tanzania mgodi wetu una juhudi za kuunga mkono serikali katika swala la kuboreha Afya ya kila mwanajamii ili kuhakikisha anaafya nzuri kwa lengo la kushiriki na kujiletea maendeleo aliongeza kusema Shayo.
Kwa upasnde wake meneja mahusiano ya jamii endelevu,Robert Ojendo alisema kuwa mamia ya watu wanaogunguka mgodi wanakabiliwa na matatizo ya macho lakini hawana uwezo wa kufika katika vituo vya kutolea huduma kutokana na uwezo mdogo wa kifedha walionao.
“Nipende kutumia nafasi hii watu wa Nyamongo mlioipata mkaitumie vizuri kujitokeza kwa wingi ilikuja kupima na kujua matatizo mliyonayo ya macho na ikibainika kuna mmjoa wenu anahitaji msaada wa kupewa miwani atapatiwa”alisema Ojendo.
Naye Mganga mkuu wa mkoa Mara,DKT Fransins Mwanisi alisema kuwa kati ya mwaka 2010 hadi 2017 kampuni ya mgodi wa kuchimba madini ya dhahabu ACACIA uliopo Nyamongo umetumia dola za kimarekani milioni 1.6 katika kutekeleza miradi ya Afya katika maeneo mbalimbali.
Na Godfrey Leonard.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WATU ZAIDI YA 3,000 KUNUFAIKA NA UPIMAJI BURE WA MACHO
Reviewed by By News Reporter
on
10/04/2018 07:07:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: