Loading...

VIGOGO WA CCM WALIONUSURIKA KUFUKUZWA, WARUDISHWA KUNDINI

Loading...
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imewarudisha kundini wanachama wake wanne waliokuwa kwenye orodha ya kuvuliwa uanachama kutokana na utovu wa nidhamu, akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.

Wengine waliosamehewa jana ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwirasa, aliyekuwa Mwenykiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge.

Uamuzi wa Halmashauri Kuu ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wake, Dk. Bashiru Ally, muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao chake kilichoongozwa na Mwenyekiti Rais John Magufuli.

“Kwa kauli moja Halmashauri Kuu wa CCM Taifa, imepokea maombi na kukubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama kutoka kwa waliokuwa wana CCM wanne ambao walitenda makosa hayo wakiwa wenyeviti wa CCM ngazi za mikoa na wilaya," alisema.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
VIGOGO WA CCM WALIONUSURIKA KUFUKUZWA, WARUDISHWA KUNDINI VIGOGO WA CCM WALIONUSURIKA KUFUKUZWA, WARUDISHWA KUNDINI Reviewed by By News Reporter on 12/19/2018 09:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.