Loading...
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mara, imewahukumu kwenda jela miaka 360 watu wanne kila mmoja kutumikia kifungo hicho, baada ya kukutwa na hatia kwa makosa 12 ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Waliohukumiwa ni Saimon Chacha (30) mkazi wa kijiji cha Rebu wilayani Tarime, Chacha Nyaila (22) mkazi wa kijiji cha Nyanungu wilayani Tarime, Zephania Mabula (44) mkazi wa Kijiji cha Kitalamanka wilayani Butiama na Bhoke Mwita (37) mkazi wa Shirati wilayani Rorya.
Akisoma hukumu hiyo jana ya kesi ya jinai namba 55 ya mwaka 2017, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mara, Stanley Mwakihaba, alisema watuhumiwa hao walitenda kosa la unyany'anyi wa kutumia silaha Septemba 2, 2016 katika Kijiji cha Magunga wilayani Butiama, majira ya usiku wakiwa na bunduki aina ya SMG, panga na shoka katika nyumba ya kulala wageni iliyopo katika kijiji hicho.
Alisema walipora kiasi cha Sh. 2,357,000 kutoka kwa watu 12, simu 2 za mkononi na kumjeruhi kwa kumpiga risasi Jenepher Howard.
Na Mary Mkeu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WANNE WAFUNGWA JELA MIAKA 360 KWA UNYANG'ANYI
Reviewed by By News Reporter
on
12/24/2018 12:07:00 PM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/24/2018 12:07:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: