Loading...

ISRAEL YATUMA BIBLIA TAKATIFU MWEZINI

Loading...
Jerusalem.Israel imetuma chombo chake cha kwanza mwezini, lakini tofauti na mataifa mengine yaliyowahi kufanya hivyo, taifa hilo limeweka kitabu kitakatifu cha Biblia.

Chombo hicho kilichorushwa Ijumaa, kinaitwa Beresheet na kimebebwa na roketi ya Marekani inayoitwa Falcon 9 ya kampuni binafsi ya Marekani ya SpaceX. Falcon (itaibeba Beresheet hadi katika uzingo wa dunia ambako itakiachia kianze safari kwa kutumia injini yake.

Chombo hicho chenye uzito wa kilo 585 kitasafiri kwa wiki saba kabla ya kutua mwezini Aprili 11.

Wakati kikiondoka, Waziri Mkuu Benjamin Netanyau akiwa pamoja na wahandisi walikuwa wakifuatilia chombo hicho kutokea katika kituo cha kuongozea cha Israel Aerospace Industries (IAI) kilichopo Israel.

Lakini tofauti na safari nyingine za kwenda mwezini, chombo hicho kimebeba boksi maalumu la kihistoria lililo na Biblia, michoro ya watoto, kumbukumbu za manusura wa utawala wa kinazi, nyimbo za Israel na bendera ya nchi hiyo ya rangi ya bluu na nyeupe.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ISRAEL YATUMA BIBLIA TAKATIFU MWEZINI ISRAEL YATUMA BIBLIA TAKATIFU MWEZINI Reviewed by By News Reporter on 2/24/2019 10:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.