Loading...

ATCL YAWATOA HOFU WANANCHI, 'NDEGE ZETU NI TOFAUTI NA ILE YA ETHIOPIA'

Loading...
Shirika la Ndege Tanzania, (ATCL) limewatoa hofu wananchi kuwa ndege mpya zilizonunuliwa na Serikali ni Salama na kwamba ndege hizo ni toleo tofauti na ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia iliyoanguka hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu 157.

Hayo amesema Captain Saidi Hamad ambaye ni Mkurugenzi Uwendeshaji ATCL “Napenda kuwatoa hofu, hizi ndege ambazo tunazo ni toleo tofauti na hiyo ya Boeing 737 Max 8 crash, haya matoleo tuliyonayo yanatumika maeneo mablimbali duniani”

Itakumbukwa kuwa Machi 10 mwaka huu kuwa ndege ya shirika la Ethiopia aina ya Boeing 737 ilianguka Addis Ababa, mji mkuu wa nchi hiyo wakati ikielekea nchini Kenya na watu wote 157 walifariki dunia. Ndege hiyo ilianguka asubuhi majira ya saa mbili na dakika arobaini na nne kwa saa za Afrika Mashariki ikiwa na abiria 149 pamoja na wafanyakazi 8.
Na John Malogo.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ATCL YAWATOA HOFU WANANCHI, 'NDEGE ZETU NI TOFAUTI NA ILE YA ETHIOPIA' ATCL YAWATOA HOFU WANANCHI, 'NDEGE ZETU NI TOFAUTI NA ILE YA ETHIOPIA' Reviewed by By News Reporter on 3/15/2019 08:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.