Loading...

DRC: RAIS TSHISEKEDI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 700 WA KISIASA

Loading...
Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  Felix Tshisekedi  atoa msamaha kwa wafungwa wa kisiasa 700.

Wafungwa wa kisiasa wasiopungua 70 Jamhuri ya Kidemokrsaia ya Kongo wapewa msamaha wa rais  na rais Felix Tshisekedi ikiwa ni moja ya ahadi alizotoa  wakati wa  kampeni za uchaguzi  uliofanyika  nchini humo.

Felix Tshisekedi alitanjwa mshindi katika chaguzi ambazo zilifanyika.
Wafungwa walioachwa huru ni wafungwa waliokuwa wamezuiliwa na  serikali ya rais Joseph Kabila Kabange. Rais Tshisekedi amesaini msamaha huo Alkhamis na kuruhu wafungwa  wa kisiasa kuachiwa huru.

Msamaha huo umetolewa siku 100 tangu rais mpya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuingia madarakani.

Mmoja miongoni mwa wafungwa walioachwa huru yumo Firmin Yangambi  ambae alikuwa amehukumiwa  kifungo cha miaka 20 gerezani tangu mwaka 2009 akituhumiwa  kuwa hatari kwa usalama wa taifa.
Na Mary Mkeu.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DRC: RAIS TSHISEKEDI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 700 WA KISIASA DRC: RAIS TSHISEKEDI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 700 WA KISIASA Reviewed by By News Reporter on 3/15/2019 09:49:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.