Loading...

HUDUMA MPYA YA USAFIRI YAZINDULIWA DAR

Loading...
KAMPUNI mpya ya usafirishaji abiria mtandaoni ijulikanayo kama Little, imezinduliwa jijini Dar es Salaam juzi Jumamosi.

Katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena iliyopo Posta jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wadau wa usafiri na madereva.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Little, Ashishi Kruketi, alisema: “Kutokana na mahitaji ya huduma ya usafiri na kuongeza ajira kwa vijana katika Jiji la Dar es Salaam, tunayo furaha kubwa kuwatangazia kuwa tumezindua rasmi huduma hii jijini hapa.”

Naye Meneja Masoko wa Little, Katimpu Kisessa, alisema kampuni yao imeshasajili madereva 500 ambao wameshapata mafunzo ya huduma kwa wateja kutoka Little.

“Kampuni yetu imeanzishwa mwaka 2016 katika Jiji la Nairobi, kwa sasa ipo katika nchi nne ambazo ni Uganda, Kenya, Zambia na Tanzania.

“Sisi tumekuja kitofauti kabisa, siyo kama wengine, mteja anapoita usafiri wa gari, Bajaj au pikipiki, safari inapoanza basi ana uwezo wa kuangalia kiasi gani cha fedha anachotakiwa kulipa, lakini pia dereva na abiria wake tumewawekea ulinzi wa kutosha,” alisema Kisessa.
Na Timoth Fredrick.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
HUDUMA MPYA YA USAFIRI YAZINDULIWA DAR HUDUMA MPYA YA USAFIRI YAZINDULIWA DAR Reviewed by By News Reporter on 3/25/2019 07:46:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.