Loading...
Baada ya ajali ya ndege iliyosababisha vifo vya watu 157 iliyotokea hapo jana, shirika la ndege la Ethiopia limetangaza kusimamisha matumizi ya ndege aina ya Boeing "737 Max 8".
Msemaji wa shirika la ndege la Ethiopia Asrat Begashaw, ametoa taarifa akisema katika kuchukua hatua za kiusalama, shirika hilo limesimamisha matumizi ya ndege aina ya Boeing 737 Max 8 kufuatia ajali iliyotokea siku ya Jumapili iliyoihusisha aina hiyo ya ndege iliyokuwa ikitoka Addis Ababa kuelekea Nairobi.
Ndege hizo aina ya Boeing 737 Max 8 zilizosimamishwa matumizi yake idadi yake ni 4.
Katika kipindi cha miezi sita ya hivi karibuni ndege hizo aina ya 737 Max 8 zinazotengenezwa na shirika la Marekani la Boeing firmasının zimehusika katika ajali kubwa 2, jambo ambalo limesababisha uwepo mvutano kuhusu usalama wa ndege hizo.
Mwezi Oktoba mwaka jana ndege aina ya 737 Max 8 ya shirika la ndege la Indonesia ilipata ajali, ambapo watu 189 walipoteza maisha.
Ingawa mpaka sasa sababu ya ajali haijafahamika lakini ndege zote 2 zilianguka dakika chache baada ya kuruka kati ya dk 6 na 12, suala linaipa nguvu nadharia kwamba aina hiyo ya ndege ina matatizo ya kiufundi toka kiwandani.
Baada ya ajali mamlaka ya anga nchini China imetoa amri ya kwa mashirika yote ya ndege nchini humo kusimamisha matumizi ya ndege hizo aina ya Boeing 737 Max 8.
Kwa upande mwingine shirika la ndege la visiwa vya Cayman imesimamisha matumizi ya ndege zake mpya 2 za abiria aina ya Boeing 737 Max 8.

Na Haika Gabriel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KUFUATIA AJALI YA NDEGE: ETHIOPIA YASIMAMISHA MATUMIZI YA NDEGE AINA YA BOEING 737 MAX 8
Reviewed by By News Reporter
on
3/12/2019 05:50:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: