Loading...
Ndege za uchukuzi wa abiria na mizigo zilizoratibiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi Kenya zimeelekezwa kutua uwanja wa Julius Nyerere Dar es Salaam Tanzania kufuatia mgomo wa wafanya kazi wa mamlaka inayosimamia viwanja vya ndege.
Mapema asubuhi ya jana Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta wamefanya mgomo uliosababisha abiria kukwama kusafiri mjini Nairobi.
Wafanyakazi wa usafiri wa ndege wameanza mgomo kupinga mpango wa kuunganishwa shughuli za usimamizi vya uwanja huo wa ndege kati ya shirika kuu la ndege nchini Kenya Airways na mamlaka ya usimamizi wa viwanja wa ndege KAA.
Muungano wa wafanyakazi hao (KAWU) umeuliza maswali kuhusu mipango hiyo ya kuunganisha shughuli kati ya pande hizo mbili na sasa unaitisha mageuzi katika usimamizi wa Kenya Airways na shirika la usimamizi wa viwanja vya ndege KAA.
Sambamba na hilo wafanyakazi wanatuhumu na kupinga makosa yanayofanyika katika uajiri wa wafanyakazi.
Hadi sasa, Wanajeshi wa Jeshi la angani la Kenya KAF sasa wamechukua usukani wa shughuli za uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na kurejesha usafiri. Hadi kufikia sasa ndege kadhaa zimeondoka.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MGOMO WA JKIA: NDEGE ZAELEKEZWA KUTUA TANZANIA
Reviewed by By News Reporter
on
3/07/2019 08:15:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: