Loading...
Mkutano ulioandaliwa nchini Ethiopia kati ya familia za abiria walioangamia katika ajali mbaya ya ndege uligeuka kuwa vurugu baada ya maafisa wa shirika hilo kushindwa kuwapa majibu ya maswali waliohitaji.
Familia hizo zilikutana katika hoteli moja la Ethiopian Airlines na kuwachagua wasimamizi wao kusaidia katika uchunguzi zaidi.
Kikuu walichohitaji ni kupata miili ya jamaa zao walioangamia kufuatia ajali ya ndege inayomilikiwa na kampuni hiyo.
Familia hizo zilighadhabika pale maafisa wa shirika hilo walipodai kuwa hawakujua iliko miili hiyo.
Walieleza kuwa miili hiyo ilichukuliwa na maafisa wa polisi wakishirikiana na maafisa wa afya.
Jamaa hao walizua vurugu wakitaka kupewa miili yao, hapo ndipo usimamizi wa hoteli hiyo ilipochukua hatua ya kuwatimua hotelini humo kwa nguvu.
Inadaiwa kuwa miili hiyo ilihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Menelik, madai ambayo hayakuthibitishwa na maafisa wa shirika la Ethiopian Airlines.
‘’Hatupati usaidizi wowote kutoka kwa maafisa hawa, hawatupi majibu yoyote wanaopaswa kutupa wanatupita tu. Hatutaki kushinda hapa,’’ Mkenya mmoja aliyepoteza mkewe katika ajali hiyo alisema.
Kama ilivyoripotiwa mitandao ya habari kote duniani, jumla ya watu 157 walipoteza uhai wao katika ajali ya ndege ya Boeng 737 iliyotokea Ethiopia dakika tano baada ya ndege hiyo kupaa kutoka katika uwanja wa ndege wa Bolle Jumapili, Machi 10.

Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MKUTANO KATI YA WAMILIKI WA ETHIOPIA AIRLINES NA FAMILIA ZA WAATHIRIWA WAGEUKA VITA
Reviewed by By News Reporter
on
3/18/2019 08:17:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: