Loading...

NABII MWENYE UTATA NA KAULI YAKE HII YA 'UTATA'

Loading...
Katika ibaada ya Jumatatu, Februari 25, Bushiri ambaye ni Nabii kutoka Afrika Kusini, aliwaeleza wafuasi wake kuwa kamwe mwenyezi Mungu hana mamlaka yoyote ya kutawala Ulimwengu. 

Nabii huyo mwenye utata, alidai kuwa kulingana na kitabu cha Mwanzo 1:28, Mwenyezi Mungu aliwapa Adamu na Hawa mamlaka lakini baada ya wawili hao kwenda kinyume na maagizo yake walipokonywa mamlaka hayo na kupewa shetani.

Bushiri alieleza kwa kina kuhusu mahubiri yake kwa kutumia mfano wake Job kwenye Biblia kuwa, Mungu alikuwepo kwenye kiti cha enzi wakati Job alikuwa anapitia wakati mgumu.

"Sasa swali kuu ni kuwa, wakati Job alikuwa anapitia mateso hayo yote huyu Mungu alikuwa wapi-kwenye kiti cha enzi? Shida ni kuwa, kwa kweli Mungu anatazama yote yanayotendeka katika Ulimwengu huu wetu lakini hana mamlaka ya kuongoza matukio yoyote." Alisema Bushiri. 

Aidha alidokeza kuwa, kwa kuwa Mungu aliona Adamu na Hawa wameenda kinyume na maagizo yake ni vyema shetani angechukua mamlaka, hivyo basi akamtuma mwanawe Yesu Kristo afe msalabani.

Aliongeza kuwa, kupitia kifo cha Kristo basi mamlaka yalihamishiwa kwa wanadamu waweze kutawala Ulimwengu. 

Hata hivyo, alikiri kuwa ni kupitia tu kwa maombi ndipo wanadamu wanaweza kupata mamlaka hayo.
Na Frank Lubayo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
NABII MWENYE UTATA NA KAULI YAKE HII YA 'UTATA' NABII MWENYE UTATA NA KAULI YAKE HII YA 'UTATA' Reviewed by By News Reporter on 3/07/2019 07:46:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.