Loading...

SIRI YA UTAJIRI: KATIKATI YA CHANGAMOTO BADO KUNA NJIA

Loading...
Safari ya kila mmoja wetu kuelekea kule anapopataka hakika si nyepesi, kuna kila aina ya changamoto na vikwazo katikati ya safari. Kuna kujikwaa na kuanguka wakati wa safari. Lakini katika yote hayo bado tuna fursa ya kuweza kufika mwisho wa safari yetu.

Pale mambo yanapoenda ndivyo sivyo na kinyume cha matarajio ya safari yako jitahidi kutazama na kuweka mkazo katika kupata jawabu na sio kuangalia matatizo yanayokukabili. Epuka kulalamika na kunyoosha vidole kwa wengine pale mambo yanapoenda kinyume na ulivyotarajia awali.

Ishi changamoto unazokutana nazo kwa kutafuta njia bora na jawabu la matatizo yaliyo mbele yako. Epuka kujihusisha na mambo yasiyo na tija katika safari yako.

Katikati ya mawimbi ya changamoto za matatizo mbalimbali bado tuna nafasi ya kufika kule tunapohitaji kufika. 

Na Vicent Stephen.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SIRI YA UTAJIRI: KATIKATI YA CHANGAMOTO BADO KUNA NJIA SIRI YA UTAJIRI: KATIKATI YA CHANGAMOTO BADO KUNA NJIA Reviewed by GEOFREY MASHEL on 3/08/2019 07:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.