Loading...
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 5 ameaga dunia baada ya wazazi wake kujaribu kumtahiri nyumba bila msaada wa mtaalam wa matibabu.
Wakati wa kumtahiri mtoto huyo alipoteza fahamu huko Bologna, Italy, kwakufanyiwa tohara ya kienyeji. Alifikishwa hospitalini siku ya Ijumaa mchana lakini alifariki usiku baadae, kwa mujibu wa vyanzo vya eneo la tukio.
Wazazi wake wamejikuta hatiani kwa kesi ya kuua bila kukusudia.
Hii inafuatia baada ya tohara ya kienyeji aliyofanyiwa kichanga wa chini ya miaka 2 aliyefariki kwa kutokwa na damu nyingi mwezi Disemba huko Rome. Katika kesi hiyo hiyo kaka zake wawili nao manusura wafariki, pia, lakini walinusurika baada ya matibabu ya hali ya juu waliyopatiwa.
Tohara nchini Itali haifanywi na wengi wa Roman Catholic, kulingana na Metro UK. Wahamiaji wengi wa nchini humo ni wa dini ya Kiislamu na wanawafanyia tohara watoto wao kwa sababu za kimila na kidini, lakini wanashindwa kupata huduma hiyo hospitalini. Kwa kuwa, gharama za hospitali ni kubwa sana. Pia, wanafanyiwa watu wazima.
Foad Audi, mwanazilishi wa jumuia ya madaktari wageni nchini Italia (AMSI), ameiomba mamlaka hiyo kuruhusu gharama za tohara kushuka ili kila mwananchi azimudu na ipatikane hata kwa watoto wa umri mdogo ili kupunguza vifo vitokanavyo na tohara za kienyeji.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

TOHARA ILIVYOMTOA UHAI MTOTO WA MIAKA 5, WAZAZI WAKE HATIANI
Reviewed by By News Reporter
on
3/26/2019 10:26:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: