Loading...

JINSI BINTI WA MIAKA 10 WA NCHINI KENYA ALIVYOALIKWA IKULU NA RAIS MUSEVENI

Loading...
Msichana mwenye umri wa miaka 10 kutoka Mombasa amealikwa na Rais Yoweri Museveni katika ikulu nchini Uganda 

Sheila Sheldone na wazazi wake wanaishi kwenye makazi ya kifahari ya jumba la Nyali Golf View ambapo pia rais Museveni alipatiwa chumba cha kulala wakati alikuwa ziarani Kenya. 

Sheila ambaye ni mchoraji hodari, alimzawadi rais Museveni na picha alomchora Jumatatu April 1 ambayo ilimfurahisha sana na kumfanya ampatie mwaliko katika ikulu.

Hii sio mara ya kwanza kwa Sheila kutambuliwa na viongozi mashuhuri kwani tayari alishapatiwa ufadhili wa masomo na rais Uhuru Kenyatta kufuatia umahiri wake wa uchoraji.

Jumba wanamoishi Sheila lina ghorofa 130, mgahawa wa kifahari, chumba cha marais kulala na bwawa la kuogelea. 

Sheila yuko katika darasa la tano katika shule ya msingi ya Light International mjini Mombasa.
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JINSI BINTI WA MIAKA 10 WA NCHINI KENYA ALIVYOALIKWA IKULU NA RAIS MUSEVENI JINSI BINTI WA MIAKA 10 WA NCHINI KENYA ALIVYOALIKWA IKULU NA RAIS MUSEVENI Reviewed by By News Reporter on 4/03/2019 10:55:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.