Loading...

KUTANA NA NABII MVAA CHUPI AKIWA ANAHUBIRI KANISANI

Loading...
Nabii mmoja kutoka nchi ya Ghana aliwaacha wengi vinywa wazi baada ya kuvaa nguo za kike wakati akiwahubiria waumini wake.

Mchungaji huyo kwa jina Kofi Oduro aliyavaa mavazi hayo juu ya mavazi yake rasmi huku akizunguka kanisani humo wakati wa ibada.

Kulingana na picha zilizosambaa Instagram, nabii huyo alikuwa anawafunza wanawake jinsi ya kunadhifisha ndoa yao na kuifanya iwe ya kufana wakiwa katika chumba cha kulala na wapenzi wao. 

Hivyo basi, katika hali ya kusisitiza kiini cha mafunzo yake, Kofi aliyavaa mavazi ya ndani ya wanawake ili kuhakikisha kuwa ujumbe wake umenakiliwa kisawasawa na wafuasi wake. 

Cha kushangaza ni kuwa, wanawake ambao walikuwa wamehudhuria kongamano hilo, waliketi kitako na kutulia huku wakimsikiliza kwa makini. 

"Wanawake wengi hujisahau wakati wanapooloewa. Nawashauri enyi wanawake wote mlioolewa, ili kuifanya ndoa yako iwe ya kufana, sharti uwe mchangamfu," nabii huyo alisema. 

Baada ya kuzua kioja cha kuvaa chupi, alitwaa pajama ya wanawake na kuivalia wakati uo huo akiendelea na mafunzo kuhusu ndoa bila hata aibu.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KUTANA NA NABII MVAA CHUPI AKIWA ANAHUBIRI KANISANI KUTANA NA NABII MVAA CHUPI AKIWA ANAHUBIRI KANISANI Reviewed by GEOFREY MASHEL on 4/17/2019 08:05:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.