Loading...

"Siri ya kufanikiwa ni kubeba picha ya matokeo ya mafanikio katika akili"

Loading...
"Siri ya kufanikiwa ni kubeba picha ya matokeo ya mafanikio katika akili"

Haya ni maneno ya Thoreau. Anajaribu kubainisha kuwa ili uweze kupata mafanikio katika akili yako unapaswa kujenga na kutembea na picha ya matokeo chanya kuhusu jambo unalolitaka. 

Mfano kama wewe unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa unatakiwa muda wote kuwa na ile picha inayokuonesha tayari wewe ni mfanyabiashara mkubwa, unaiona ile kampuni kubwa utakayoianzisha, unawaona wale wafanyakazi wako watakaokuwa wanafanya kazi na wewe, unaona vile vikao vikubwa vya kusaini mikataba ya uwekezaji katika nchi mbalimbali, unaona safari mbalimbali za kibiashara ambazo utakuwa unazifanya.

Tafiti zinaonesha, uwepo wa picha ya namna hii katika akili huchochea na kuongeza uwezo wa ubunifu wa akili katika kuainisha mikakati mbalimbali ya kufanikisha kile kilicho ndani yake. Hamasa ya kujituma na kuchukua hatua ili kufanikisha matokeo ya ile picha iliyo ndani pia huongezeka.

Je una picha yoyote ya matokeo chanya ya kile unachokita katika akili yako? Ukijitazama unaona nini ndani yako? Unaona sawa sawa na kile unachokitaka au unaona mtu wa aina nyingine?.

Keep Moving ! One Step At A Time!
Vicent Stephen.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
"Siri ya kufanikiwa ni kubeba picha ya matokeo ya mafanikio katika akili" "Siri ya kufanikiwa ni kubeba picha ya matokeo ya mafanikio katika akili" Reviewed by By News Reporter on 4/18/2019 09:17:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.