Loading...

FAHAMU FAIDA 10 ZA KUFANYA MAZOEZI

Loading...
Watu wengi huwa na wasiwasi kuhusu uzito wao wa mwili maishani. Wengine huwa na hofu uzito wao ukipungua ghafla ama ukiongezeka. 

Kulingana na ripoti ya shirika la afya duniani WHO, na iliyochpishwa na The Citizen, takriban watu billioni 1.9 wanaugua ugonjwa wa sukari ama uzito wao kuongezeka maradufu. Shirika hilo pia lilipendekeza kufanya mazoezi kila mara kama njia bora ya kuimarisha afya na kudhibiti uzito.

Lakini je unajua faida za kufanya mazoezi? Basi hii hapa orodha ya faida za kufanya mazoezi:

1. Kuzuia Magonjwa yasiyoambukizana

Kufanya mazoezi yanasaidia kuzuia magonjwa yasiyoambukizana kama vile saratani, mshtuko wa moyo na kisukari. Mazoezi pia yanasaidia moyo kuwa na kazi rahisi ya kusukuma damu. 

2. Kudhibiti uzito wa mwili 

Uzito wa mwili kupita kiasi ni athari kubwa ya kupata magonjwa yasiyoambukizana . Lakini kwa kufanya mazoezi, mwili hupata kusisimuka kwa hivyo kumaliza mafuta yaliyo ganda kwenye mishipa.

3. Kupunguza presha

Mazoezi husaidia kudhibiti mishipa ya damu na pia kuchangia kudhibiti presha ambayo ni athari kubwa kwa mpigo wa moyo.

4. Kusaidia mfumo wa kupumua 

Mazoezi rahisi kama vile kutembea, kukimbia na kuogelea husaidia misuli kuwa na nguvu yakusambaza hewa safi na kutoa hewa chafu.

5. Kupunguza athari ya kupata saratani 

Utafiti unaonesha kuwa kufanya mazoezi hupunguza athari za kupata saratani ya matiti na mapafu.

6. Kudhibiti 'cholestorol' mwilini 

'Cholesterol ' ni mafuta mwilini yanayojihifadhi kwenye mishipa ya damu. Mazoezi husaidia kuondoa yale mafuta sumu mwilini na kuongeza yale muhimu.

7. Mifupa kuwa na nguvu 

Mazoezi husaidia mifupa kuwa na nguvu kuepuka athari za kupata magonjwa ya mifupa kama vile oesteoporosis. Ugonjwa huu husababisha mifupa kupungua makali.

8. Kuboresha akili 

Mazoezi husababisha mwili kutoa kemikali kwa jina 'endophin' inayosaidia mwili kuchangamka na kuleta kufuraha. Pia hukinga akili kutokuwa na mawazo machafu na pia kuzuia mawazo mengi kwa hivyo kufanya mtu kuwa jasiri.

9. Kuondoa sumu na kudhibiti joto mwilini 

Wakati wa mazoezi mwili hutokwa na jasho jingi sana ikiwemo sumu iliyokuwa mwilini na maji, mwili pia huwa na joto jingi. Kwa hivyo mazoezi husaidia kuhifadhi joto mwilini.

10. Kuboresha afya ya ngozi 

Mazoezi husababisha ngozi kuwa safi na yenye afya. Ngozi pia huonekana changa.
Na Saidi Nzela.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
FAHAMU FAIDA 10 ZA KUFANYA MAZOEZI FAHAMU FAIDA 10 ZA KUFANYA MAZOEZI Reviewed by By News Reporter on 5/16/2019 10:27:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.