Loading...
Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari linaendelea mjini Bonn na siku ya kwanza mjadala mkubwa umetuama juu ya nafasi ya mitandao ya kijamii ambayo katika miaka ya karibuni imekuwa kitovu cha upatikanaji habari.
Hata hivyo mitandao ya kijamii imegeuka kuwa chanzo cha wasiwasi wa kusambaa kwa habari za uzushi na upotoshaji.
Katika majadiliano ya wazi yaliyowajumuisha wawakilishi wa vyombo vya habari na afisa kutoka kampuni ya Facebook suala la kuongezeka kitisho cha kusambaa habari za uzushi na upotoshaji limeibuka kuwa changamoto kubwa kabisa zama za mapinduzi ya teknolojia.
Mkurugenzi wa kampuni ya habari kupitia mtandao ya Axel Springer, Mathias Döpfner, ameyalaumu makapuni makubwa ya mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook na Google kwa kutochukua hatua madhubuti kukabiliana na kitisho cha habari bandia.
Kampuni hizo zimelaumiwa kwa kushindwa kuweka mifumo kamili ya usalama ikiwa ni pamoja na kuzuia kusambaa kwa taarifa za uuzushi na kuchukua hatua za kupunguza uwepo wa akaunti bandia zinazoendesha shughuli za kusambaza chuki na taarifa za uongo.
Mhariri mkuu wa jarida la India Today Aroon Purie amesema changamoto kubwa ni kuwa makampuni yanayomiliki mitandao ya kijamii yamegeuka kuwa biashara badala ya kufanya kazi ya kutoa huduma na kusaidia jamii.

Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
HABARI ZA UZUSHI ZAWA TISHIO, LAWAMA WATUPIWA MITANDAO YA KIJAMII
Reviewed by By News Reporter
on
5/28/2019 07:29:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: