Loading...
Kenya. Sala ilikatizwa ghafla na kugeuka shubiri kwenye msikiti mmoja Taita Taveta baada ya jamaa kutoka Afrika Kusini kuvamia eneo hilo jana Jumatano, Mei 29.
Kulingana na kamanda wa kaunti hiyo Lawrence Marwa, mwekezaji huyo wa kigeni ambaye anaishi katika jengo moja karibu na kijiji cha Mata, aliwavamia watu waliokuwa wamekusanyika msikitini humo kwa maombi ya asubuhi.
Baada ya kuwasili mahali hapo, mshukiwa huyo alilalamikia kuhusu kelele na akaelekea katika ukumbi wa msikiti huo na kukata nyaya za kipaza sauti, kulingana Standard ilivyoripoti.
Katika muda huo wote mshukiwa alizunguka akionesha bastola yake hewani.
"Mshukiwa aliwasili katika msikiti huo na kuwaamuru waliokuwa wakiabudu kupunguza sauti ya vifaa vya kuwasilisha ujumbe. Tumemkamata mshukiwa na atafunguliwa mashtaka ya kuwasumbua wananchi," Marwa alifichua.
Marwa alidokeza kwamba, maafisa wa polisi walipokea ripoti kuhusu tukio hilo na waliwasili mahala hapo na kumkamata mshukiwa.
Mshukiwa huo pia atachunguzwa iwapo yupo humu nchini kihalali.
Wazee wa misikiti wamekashifu kitendo hicho na kusema kwamba silaha haziruhusiwi mahala pa sala.

Na Ummy Kitwana.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIA WA AFRIKA KUSINI AANZISHA KITIMTIM MSIKITINI WAKATI WA SALA
Reviewed by By News Reporter
on
5/30/2019 08:12:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: