Loading...

SIRI YA UTAJIRI: JARIBU KUDHARAU MANENO UNAYOSEMWA, MUNGU AMEKUUMBA KWA KUSUDI MAALUM

Loading...
Watu wengi tumeumizwa na maneno mabaya ambayo watu wanatusema na wakati mwingine na matendo mabaya ambayo wanatutendea. 

Katika hali hii kuna watu wamefikia hatua ya kuamini kile wanachoambiwa na kusemwa na wengine kiasi cha kukataa tamaa na maisha yao.

Kuna kitu kimoja usichokijua, Mwenyezi Mungu alikuumba kwa kusudi maalum na uwepo wako katika dunia hii ni kwa ajili ya kukamilisha kusudi hilo. Wewe ni wa thamani kubwa mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu.

Usiruhusu kile wanachokusema watu ama wanachokutenda kuainisha ulivyo. Hivyo ulivyo ni sawa sawa na mapenzi ya Mungu, usikubali mtu mwingine akuambie vinginevyo. Pamoja na maneno yao endelea kukuza na kujenga kile ambacho kiko ndani yako kwa ajili ya kukamilisha lile kusudi kuu ambao limewekwa ndani yako. 

Kwa kuishi na kutembea katika njia iliyotengenezwa kwa ajili yako utaishi maisha ya furaha na utoshelevu. Maneno, uongo, majungu na nia mbaya za watu zisikufanye ukapoteza mwelekeo wa kile ambacho umekusudiwa. 

Pamoja na yote haya, Usisahau kuwatendea watu wengine katika namna ile ile ambayo ungependa wewe utendewe.

Keep Moving ! One Step At A Time !!
Vicent Stephen
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SIRI YA UTAJIRI: JARIBU KUDHARAU MANENO UNAYOSEMWA, MUNGU AMEKUUMBA KWA KUSUDI MAALUM SIRI YA UTAJIRI: JARIBU KUDHARAU MANENO UNAYOSEMWA, MUNGU AMEKUUMBA KWA KUSUDI MAALUM Reviewed by By News Reporter on 5/28/2019 07:47:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.