Loading...
Mkazi wa Ndembezi Shinyanga Mjini, Ester Samwel (35), ameuawa kwa kupigwa na wananchi baada ya kutuhumiwa kuiba mboga aina ya spinachi mafungu sita, nyanya debe moja na mahindi mabichi matatu.
Tukio hilo lilitokea juzi maeneo ya Kitangili, Shinyanga Mjini, wakati Ester alipodaiwa kuiba kwenye sokoni na wananchi kupiga kelele za mwizi na kumshambulia kwa kipigo hadi kusababisha kifo chake.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jana, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Richard Abwao, alisema wananchi hao baada ya kumshambulia Ester, alikosa nguvu na hatimaye kukimbizwa hospitali ya rufani ya mkoa na kufariki dunia.
"Chanzo cha mauaji ya mwanamke huyu ni wananchi kujichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu marehemu kuiba mboga aina ya chinese mafungu sita, nyanya debe moja pamoja na mahindi mabichi matatu," alisema Abwao na kuongeza:
"Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinyanga, na juhudi za kuwasaka watu waliohusika na mauaji hayo zinaendelea."

Na Catherine Lameck.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AAGA DUNIA KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAFUNGU 6 YA MBOGA ZA MAJANI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
6/22/2019 08:48:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: