Loading...
Mwanamke mmoja nchini Ethiopia amefanya mtihani hospitali dakika 30 baada ya kujifungua
Almaz Derese , mwanamke mwenye umri wa miaka 21 kutoka mkoa wa Metu nchini Ethiopia alikuwa na matarajio ya kufanya mitihani kabla ya kujifungua , lakini mitahani ya shule za upili nchini Ethiopia iliahirishwa kutokana na mwezi wa Ramadhani.
Almaz Derese alipatwa na uchungu wa kujifungua Jumatatu muda mchache kabla ya mtihani huo wa taifa kuanza.
Almaz Derese amesema kuwa kusoma akiwa mjamzito haikuwa tatizo na hakutaka kusubiri baada ya mwaka mmoja ndio afanye mtihani huo.
Alifanya mtihani wa lugha ya kiingereza, hisabati na lugha ya Amhariki akiwa hospitali na kumalizia mitihani iliosalia katika kituo kilichoandaliwa kwa ajili ya mitihani hiyo ya taifa Alkhamisi Juni 13.
Mume wa Derese aliwashawishi wasimamizi wa mitihani kumruhusu mkewe kufanya mitihani yake akiwa hospitali.
Ni jambo la kawaida nchini Ethiopia mwanamke mjamzito kusimamisha masomo na kurejea shuleni baada ya kujifungua.

Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AFANYA MTIHANI DAKIKA 30 BAADA YA KUJIFUNGUA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
6/13/2019 08:21:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: