Loading...

EBOLA YAIBUKIA NCHINI UGANDA, MTOTO ATHIBITIKA KUAMBUKIZWA VIRUSI

Loading...
Mtoto wa miaka mitano nchini Uganda apatikana kuwa na Ebola, shirika la afya duniani (WHO) limethibitisha.

Hiki ni kisa cha kwanza kuthibitishwa katika nchi hiyo wakati kukishuhudiwa mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo.

Zaidi ya visa 2,000 vimenakiliwa huko katika muda wa miezi 10 iliyopita - wengi wa waathirika wakifariki.

Inaarifiwa kuwa mtoto huyo wa kivulana alisafiri na familia yake na kuvuka mpaka kutoka Congo siku ya Jumapili.

Baada ya hapo alipelekwa katika hospitali moja nchini Uganda baada ya kuonyesha dalili ikiwemo kutapika damu, maafisa wamesema.

Uthibitisho kwamba ni ugonjwa wa Ebola ulitolewa na taasisi ya kupambana na virusi nchini Uganda Virus Institute (UVRI) jana Jumanne kal aya kutangazwa rasmi na maafisa jana usiku.

Waziri wa afya Uganda Jane Ruth Aceng amewaambia wanaandishi habari kwamba familia ya mtoto huyo wanaangaliwa, wakiwemo wawili walionyesha kuwa na dalili za kama za ugonjwa wa Ebola.

Baada ya hapo alituma ujumbe kwenye Twitter akieleza kwamba nchi hiyo imeingia katika 'hali ya muitikio'kufuatia kisa hicho.

Tayari wahudumu 4, 700 nchini Uganda wamepewa chanjo dhidi ya ugonjwa huo, taarifa hiyo ya pamoja ya shirika la afya duniani na wizara ya afya nchini imeendelea kueleza.

Mlipuko huo katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ni wa pili kwa ukubwa katika historia, huku kukishuhudiwa ongezeko la visa vipya katika wiki za hivi karibuni.

Takriban watu 1,400 wamefariki kutokana na ugonjwa huo tangu Agosti.

Ni mara moja tu ambapo ugonjwa huo umewahi kuendelea kuwa na makali zaidi ya miezi minane baada ya kuanza - na lilikuwa janga lililoshuhudiwa Afrika magharibi kati ya mwaka 2013 na 2016 lililosababisha vifo vya watu 11, 310.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
EBOLA YAIBUKIA NCHINI UGANDA, MTOTO ATHIBITIKA KUAMBUKIZWA VIRUSI EBOLA YAIBUKIA NCHINI UGANDA, MTOTO ATHIBITIKA KUAMBUKIZWA VIRUSI Reviewed by By News Reporter on 6/12/2019 09:21:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.