Loading...

IRAN YAJIBU VITISHO VYA TRUMP, 'HII SIO KARNE YA 18'

Loading...
Jawad Zarif , waziri wa mambo ya nje wa Iran ajibu vitisho vya rais wa Marekani Donald Trump kwa kusema kuwa Marekani haina uwezo wa kuidhuru Iran.

Akihojiwa kuhusu vitisho vya Marekani dhidi ya Iran waziri wa mambo ya nje wa Iran Jawad Zarif  na kituo cha habari cha CNN mjini Tehran, Zarif amesema kuwa  Marekani haina uwezo wa kuidhuru Iran.

Zarif katika mahojiano hayo amesema kuwa Marekani haina uwezo wa kuidhuru Iran kama haitotumia silaha za maangamizi  ya halaiki zilizopigwa marufuku.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran ameendelea akisema kuwa rais Trump anatakiwa  kufahamu  kuwa  karne ya 18 imekwishapita na vitisho vya vita ni kinyume na  sheria za Umoja wa Mataifa.
Na Geofrey Okechi.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
IRAN YAJIBU VITISHO VYA TRUMP, 'HII SIO KARNE YA 18' IRAN YAJIBU VITISHO VYA TRUMP, 'HII SIO KARNE YA 18' Reviewed by By News Reporter on 6/30/2019 06:34:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.