Loading...

UN: MAPIGANO YA KIKABILA DRC, 'YARUDISHA NYUMA JUHUDU ZA KUPAMBANA NA EBOLA'

Loading...
Zaidi ya watu 300,000 wametoroka makwao mwezi huu kufuatia ghasia za kikabila katika mkoa wa Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Umoja wa Mataifa unasema.

Kuna hofu huenda makabiliano ya hivi karibuni kati ya - Wahema ambao ni wafugaji na Walendu ambao ni wakulima - huenda yakaathiri juhudi za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola katika eneo hilo.

Jamii hizo mbili zimekuwa zikizozania ardhi na maji mkoani Ituri pamoja na dhahabu katika eneo la Kaskazini -Mashariki.

Uhasama kati ya jamii hizo mbili ulisababisha vifo vya maelfu ya watu kati ya miaka ya 1997 na 2003.

Mwaka 2012,mbabe wa kivita kutoka jamii ya Hema alijihusisha na machufuko, Thomas Lubanga, alikuwa mtu wa kwanza kushitakiwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai (ICC).

Mwaka 2017, kiongozi wa wanamgambo wa Walendu, Germain Katanga, alikuwa wa kwanza kushitakiwa kwa uhalifu wa kivita na kuamriwa na ICC kuwalipa fidia waathiriwa wake became the first convicted war criminal to be ordered to pay damages to his victims by the ICC.

Jumla ya watu milioni sita waliuawa wakati wa mapigano ya miaka sita ya vita nchini DR Congo. Wengi wa waliofariki walikua na magonjwa na ukosefu wa lishe bora.

Mataifa kadhaa jirani pia yalihusika katika mapigano hayo yaliyotanjwa na walioshuhudia kama "vita vikuu ya Africa".

Karibu watu 160 wameripotiwa kuuawa katika mapigano ya sasa mkoani Ituri. Wengi wa waathiriwa wanaaminiwa kutoka jamii ya Wahema.

Chanzo halisi cha mapigano haijabainika huku wale waliotoroka makwao wakiungana na jamaa zao au kuingia kwenye kambi ambako hali kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa . (UNHCR) ni ''mbaya".

Msemaji wa UNHCR Babar Baloch tamewaambia wanahabari mjini Geneva kuwa shirika hilo jilimesikitishwa na ripoti za hivi punde na kuhofia kuwa ghasia inaendelea kusambaa katika maeneo mengine mkoani humo. ".

Bw. Balochamesema kuwa shirika hilo limepokea ripoti ya idadi kubwa ya watu waliotoroka mwakwao katika maene matatu kati ya matano ya utawala wa mkoa wa Ituri ikiwa ni pamoja na - Djugu, Mahagi na Irumu.

"Watu wanatoroka mapigano katika eneo la Djugu, huku jamii zote mbili zikisemekana zimebuni makundi ya kijilinda ambayo yanafanya mauaji ya kipiza kisasi,"alisema.

Pia aliongeza kuwa kumeripotiwa visa vya utekaji nyara watu kukatwa viungo vyao vya mwili na unyanyasaji wa kingono, katika maeneo ambayo mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu kama vile UNHCR na mashirika mengine hayawezi kufika maeneo yalioathiriwa.

Idadi kubwa ya watu wanaotoroka makwao huenda wakaathiri juhudi za kudhibiti na mambukizi ya ugonjwa wa Ebola katika eneo hilo. Msemaji wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, amewaambia wanahabari.

Tarik Jasarevic amesema ni vigumu kufuatilia hali ya watu kila siku kulingana na mwongozo wa matibabu wa siku 21 ambayo viini vya ugonjwa huo huweza kugunduliwa kwasababu watu hawatulii mahali pamoja.

Zaidi ya watu 1400wamefariki kutokana na mlipuko wa hivi karibuni wa Ebola ambao unatajwa kuwa mkubwa zaidi katika historia

Mlipuko wa ugonjwa huo umegunduliwa katika eneo la Mashariki mwa DR Congo, japo visa vingine vya maabukizi vimeripotiwa katika nchi jirani ya Uganda

Karibu 10% ya vifo vilivyotokana na maradhi ya Ebola imeripotiwa mkoani Ituri, alisema Jasarevic.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UN: MAPIGANO YA KIKABILA DRC, 'YARUDISHA NYUMA JUHUDU ZA KUPAMBANA NA EBOLA' UN: MAPIGANO YA KIKABILA DRC, 'YARUDISHA NYUMA JUHUDU ZA KUPAMBANA NA EBOLA' Reviewed by GEOFREY MASHEL on 6/19/2019 07:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.