Loading...

AFCON 2019: ALGERIA, TUNISIA ZATINGA NUSU FAINALI

Loading...
Jana ilikuwa patashika katika michuano ya AFCON katika michezo ya robo fainali ambapo timu ya Algeria kushinda kwa mikwaju ya penati 3 - 4, baada ya dakika 90 na dakika za nyongeza kwa timu zote mbili kuonyeshana ubabe kwa kufungana Ivory Coast 1 - 1 Algeria. Algeria inafikiwa kutinga fainali tangu mwaka 2010 na huku ikiweka rekodi ya kutofungwa toka michuano ianze (shinda 4, droo 2)

Mchezo mwingine ulikwa kati ya Madagascar dhidi ya Tunisia, ambapo mchezo ulimalizika kwa Tunisia kumfunga kibonde wake goli tatu bila majibu. Magoli yote ya Tunisia yamefungwa dakika 45 za kipindi cha pili na wachezaji kama Ferjani 52', Youssef Msakni 60' na Naim 90'.

Mzunguko wa robo fainali ndio umekamili na sasa timu zilizofu zinajiandaa kwa michezo ya nusu fainali ambapo timu ya Senegal itakiminya na Tunisia na Algeria itakiminya na Nigeria.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AFCON 2019: ALGERIA, TUNISIA ZATINGA NUSU FAINALI AFCON 2019: ALGERIA, TUNISIA ZATINGA NUSU FAINALI Reviewed by By News Reporter on 7/12/2019 05:34:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.