Loading...
Mwanamume mmoja raia wa Uingereza aliyenusuruka kifo baada ya mwili kudondoka kutoka kwa ndege ya shirika la Kenya Airways (KQ), ametoweka nyumbani kwake, siku moja tu baada ya kisa hicho.
Jamaa huyo, John Baldock, alikuwa akipunga hewa kwenye bustanini mwake kabla ya starehe zake kukatizwa ghafla na tukio hilo.
Baldock, ambaye ni mhitimu kutoka chuo kikuu cha Oxford, alikuwa amepangisha nyumba hiyo iliyoko katika mtaa wa Clapham, Uingereza Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa za The Sun, Baldock ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa mpangishaji, alishtuka sana baada ya mwili huo kuanguka karibu na mahali alipokuwa amepumzika.
Jirani yake ambaye alishuhudia kisa hicho alidai kuwa mwili huo ulianguka kwa kishindo kikubwa sana hadi kuyumbisha jiko lake.
"Nilifikiri nyumba yangu ilikuwa inang'oka. Nilichungulia kwenye dirisha na kuona mwili huo. John alikuwa nje akipunga upepo. Ni mpangaji na pia rafiki yake Bob mpangishaji. Nilimwona John kule nje akiwa anatetemeka sana hadi kushindwa kuzungumza," alisema jirani huyo kama alivyonukuliwa na The Sun.
Kwa sababu ya kisa hicho cha kushtusha na pia kunusirika kifo, John aliamua kurejea nyumbani kwao Exter, Devon.
Mwili huo, ulidondoka kutoka kwenye ndege hiyo dakika chache tu kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Heathrow nchini Uingereza. Inaaminika kuwa marehemu alikuwa amejificha kwenye ndege hiyo kwa saa tisa kutoka Nairobi hadi Uingereza.
Jambo ambalo lilimuogopesha zaidi John, ni kuwa mwili huo ulikuwa umepondeka vibaya sana kwa sababu ya kuanguka kwa kishindo.
Hii ilikuwa ishara tosha kuwa endapo mwili huo ungemwangukia, basi asingeli nusurika kifo.
"Mwili huo ulianguka karibu na yeye na ulikuwa umeathirika vibaya sana. Rafiki yangu alishtuka sana." alisema rafiki yake mmoja.
Ndege hiyo ilikuwa umbali wa futi 3500 angani na ulikuwa waenda mwendo wa kilomita 322 kila dakika huku ikijitayarisha kutua.
Bado haijabainika ikiwa mwili huo ulikuwa wa Mkenya kwani alikosa stakabathi muhimu za kumtambua.

Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JAMAA ATOWEKA BAADA YA MWILI KUTOKA KWENYE NDEGE YA KENYA AIRWAYS KUANGUKA NYUMBANI KWAKE
Reviewed by By News Reporter
on
7/04/2019 07:25:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: