Loading...

KISA CHA JAMAA ALIYEFUFUKA WAKATI WA MAZISHI YAKE

Loading...
Kulishuhudiwa kizazaa kwenye mtaa mmoja nchini India baada ya jamaa aliyedhaniwa kufarika 'kufufuka' wakati wa shughuli ya mazishi yake. 

Mohammad Furqan, kutoka mtaa wa Uttar Pradesh, alikuwa amelazwa katika hospitali moja mnamo Juni 21, 2019 na akatangazwa kufariki.

Kulingana na gazeti la Hindustan Times, Furqan alikuwa mmoja wa waathiriwa katika ajali ya barabarani iliyomwacha katika hali mbaya. 

Huku akiwa amelazwa kwenye hospitali hiyo, familia yake iliiambia usimamizi wa kituo hicho cha afya kuwa hawakuwa na fedha za kugharamia malipo. Ndipo hapo famili ilijulishwa kuwa ndugu yao alikuwa 'amefariki'.

Furqan alipelekwa nyumbani na shughuli za mazishi zikaanza. 

Huku shughuli hizo zikiendelea, 'maiti' alionekana akiamka na kuzua kizazaa huku waombolezaji wakaanza kukimbia kila mmoja.

"Tulikuwa tunaendelea na shughuli za mazishi wakati ambapo tuliona maiti akiamka. Alikimbizwa katika hospitali ya Ram Manohar Lohia na madaktari wakasema hakuwa amefariki" nduguye Furqan aliambia gazeti hilo. 

Furqan inaarifiwa yuko katika hali mahututi lakini madaktari wanasema yungali hai. 

Daktari mkuu wa Lucknow Narendra Agarwal alidhibitisha tukio hilo na kusema litachunguzwa zaidi.
Na Neema Joshua.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KISA CHA JAMAA ALIYEFUFUKA WAKATI WA MAZISHI YAKE KISA CHA JAMAA ALIYEFUFUKA WAKATI WA MAZISHI YAKE Reviewed by By News Reporter on 7/09/2019 06:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.