Loading...

KWANINI BBC IMEAMUA KUFUNGA OFISI ZAKE NCHINI BURUNDI?

Loading...
Shirika la habari la BBC jana imetangaza kufunga ofizi zake nchini Burundi pamoja na shughuli zake zote nchini humo baada ya juhudi za kupata suluhu na serikali kushindikana.

Mwezi Machi, serikali ya Burundi ilipiga marufuku matangazo ya BBC nchini humo na watu wamekatazwa kutoa taarifa ya aina yeyote baada ya BBC kushutumiwa kurusha matangazo ambayo serikali ilidai yamechafua sifa ya nchi.

Sauti ya Amerika (VOA) pia ilipigwa marufuku mwezi Machi nchini humo.

Kumekuwa na hofu kubwa ndani na nje ya nchi hiyo juu ya uhuru wa habari nchini Burundi.

Wiki iliyopita, Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch lilipinga vikali uteuzi wa mkuu mpya wa Shirika la Utangazaji la nchi hiyo ambaye ni kiongozi wa kundi la wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali.

Mwezi Machi mwaka huu, Baraza la Kitaifa la Mawasiliano nchini Burundi liliwapiga marufuku waandishi wa BBC na wale wa VOA kutofanya kazi nchini humo.

Baraza lilisema kuwa halimruhusu mwandishi yeyote , akiwa raia wa Burundi ama yule wa kigeni kutoa habari yoyote kwa mashirika hayo ya habari.

Amri hiyo ilitokana na kile kilichoitwa na mamlaka makala ya uongo ya BBC mwaka uliopita kuhusu mauaji yaliotekelezwa na vikosi vya usalama katika nyumba ya siri ndani ya mji mkuu wa Bujumbura.

Mamalaka nchini Burundi imesema kuwa makala hayo yalikiuka sheria za habari nchini humo.

BBC imeendelea kusisitiza kuwa makala hayo yalifuata taratimu zote za kiuandishi na kutetea waandishi wake.
Na Everlin Francis.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KWANINI BBC IMEAMUA KUFUNGA OFISI ZAKE NCHINI BURUNDI? KWANINI BBC IMEAMUA KUFUNGA OFISI ZAKE NCHINI BURUNDI? Reviewed by By News Reporter on 7/17/2019 07:39:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.