Loading...

MABAKI YA KIUMBE KILICHOISHI MIAKA MILIONI 70 ILIYOPITA YAGUNDULIWA

Loading...
Wafanyakazi wa mgodi mmoja nchini Kanada wamegundua na mabaki ya kiumbe aina ya reptilia wa majini anayesadikiwa kuishi miaka milioni 70 iliyopita.

Mkurugenzi wa makumbusho katika jimbo la Alberta, Dan Spivak, amearifu kwamba wafanyakazi katika mgodi mmoja uliokaribu na Lethbridge wamepata mabaki ya kiumbe wa zamani ambaye tofauti na Dinasor, kiumbe hicho kinasadikiwa kuishi majini.

Spivak alisema kiumbe hicho cha kutisha kilikuwa na ukubwa kati ya mita 6.5 hadi 7, fuvu la kiumbe hicho lilikuwa na ukubwa wa mita 1 likiwa na meno yaliyochongoka. Hivi sasa hakuna kiumbe chochote kinachoishi duniani kinaweza kufananishwa na kiumbe hicho.
Na Paskali Joseph.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MABAKI YA KIUMBE KILICHOISHI MIAKA MILIONI 70 ILIYOPITA YAGUNDULIWA MABAKI YA KIUMBE KILICHOISHI MIAKA MILIONI 70 ILIYOPITA YAGUNDULIWA Reviewed by By News Reporter on 7/04/2019 06:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.