Loading...

RAIS MAGUFULI KUZINDUA HIFADHI YA TAIFA MPYA HUKO CHATO

Loading...
Rais John  Magufuli anatarajiwa kuzindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Burigi huko Chato siku ya Jumanne Julai 9,  mwaka huu, ambayo imepandishwa hadhi hivi karibuni kutoka lililokuwa pori la akiba la Burigi, ambapo pamoja na mambo mengine, atakabidhi vibali na hati kwa wawekezaji mbalimbali ili kuwekeza katika eneo hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala,  amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari wanaokutana jijini Mwanza katika mkutano ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) ukiwa na kauli-mbiu ya miaka 60 ya shirika hilo katika kuimarisha uhifadhi na kupanua wigo na fursa za utalii kusini-magharibi na kaskazini-magharibi mwa Tanzania.

Dkt.  Kigwangala amebainisha kuwa uzinduzi wa hifadhi hiyo mpya una nia ya kufungua eneo hilo badala ya ule wa kaskazini pekee uliozoeleka.

Amebainisha kuwa sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika ukuaji wa pato la taifa kutokana na kuingiza fedha nyingi za kigeni ikilinganishwa na sekta zingine ambapo kwa sasa sekta hiyo inachangia asilimia 17.6 kwenye pato la taifa.
Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAIS MAGUFULI KUZINDUA HIFADHI YA TAIFA MPYA HUKO CHATO RAIS MAGUFULI KUZINDUA HIFADHI YA TAIFA MPYA HUKO CHATO Reviewed by By News Reporter on 7/05/2019 06:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.