Loading...
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameeleza kuridhishwa na jitihada zinazochukuliwa na Manispaa ya Ilala kuhusiana na ugonjwa wa Dengue huku akiwataka wananchi kuwajibika katika kuhakikisha wananunua dawa ya kuteketeza mazalia ya mbu wanaosababisha ugonjwa huo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagrama aliandika: "Leo nimefanya ziara mkoani Dar es salaam, @ilalamanispaa ili kukagua utekelezaji wa maelekezo niliyotoa kwa Mikoa/Halmashauri ya kupambana na ugonjwa wa Dengue nchini,
" aliandika waziri Ummy.
Aliongezea: "kwa ufupi nimeridhishwa na hatua walizochukua hususani @ilalamanispaa chini ya uongozi mahiri wa Mhe DC @sophia_mjema, Mkurugenzi wa Ilala na Mbunge wa Ilala #MheMussaAzanZungu ikiwemo;-
- kununua mashine mpya 14 za kupuliza dawa (motorised sprayers) - wamenunua viuadudu kutoka kiwandani Kibaha lita 3,980 (shs 53m) - Wamenunua lita 210 za kuua mbu wapevu na
upuliziaji unaendelea ktk kata 25.
"Matokeo ya jitihada hizi yanaoneka. Idadi ya wagonjwa wa Dengue Wilaya ya Ilala imepungua kutoka wagonjwa 527 mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 207 mwezi June 2019*. Kwa ujumla, wagonjwa wa Dengue mkoa wa DSM pia wamepungua kutoka 2,759 mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 790 mwezi June," waziri Ummy aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Waziri Ummy ameongeza kuwa Serikali inajitahidi kuendelea jitihada ya kupambana kipimo huku kipimo cha ugonjwa huo kikiwa ni bure. Huku akitoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kutokomeza mbu.

Na Saida Mbaningo.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAZIRI UMMY AINGIA 'MTA KWA MTAA' KUTOKOMEZA DENGUE, ASIFU JITIHADA ZA WILAYA YA ILALA
Reviewed by By News Reporter
on
7/04/2019 06:10:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: