Loading...
Rais wa zamani wa Zimbabwe amelazwa hospitalini huko Singapore, Dundiika News imebaini.
Rais wa Zimbabwe Edward Mnangagwa alitoa taarifa kuhusu suala hilo ila hakuweka bayana maradhi anayougua Mugabe.
Hata hivyo alisema kwamba rais huyo wa zamani alikuwa akipokea matibabu na alikuwa anazidi kupata nafuu.
"Mugabe amelazwa katika hospitali moja nchini Singapore ambapo anapokea matibabu. Hapo awali rais wa zamani alikuwa akipokea matibabu kwa muda wa kama mwezi mmoja na kuruhusiwa kurejea nyumbani ila wakati huu madaktari wamependekeza alazwe kwa muda mrefu ili ashughulikiwe ipasavyo. Amekuwa huko tangu Aprili," taarifa ya Mnangagwa ilisema.
Tayari kikosi cha maafisa serikali kimetumwa katika hospitali hiyo ya nchini Singapore ili kumtembelea Mugabe na kumjulia hali.
Kikosi kilichotumwa kumwona Mugabe kilisema kwamba hali yake ya afya imeimarika na ataondoka hospitalini hivi karibuni," aliongeza.
Kumekuwa na wasi wasi kuhusu hali ya afya ya kiongozi huyo ambaye ana umri wa miaka tisini na tano huku kukiwa na fununu kwamba amepoteza uwezo wa kuzungumza.
Mugabe amekuwa hospitalini kwa miezi kadhaa huku ripoti za serikali zikionesha kwamba amekuwa anatatizika kutembea.

Na Catherine Kisese.
.
.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MUGABE YUPO HOI, ALAZWA HOSPITALINI SINGAPORE
Reviewed by By News Reporter
on
8/07/2019 08:26:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: